
Mapishi haya yanatumia mazao ya NUS ya jadi yanayochangia lishe bora kwa familia za Tanzania.
Mahitaji / Malighafi
Njugumawe, mtama ulioambuliwa au mchele, mafuta, chumvi
Maandalizi
1. Chemsha njugumawe hadi zipikike.
2. Ongeza mchele au mtama, mafuta na chumvi.
3. Koroga vizuri na pika taratibu hadi ziive. Weka mezani ikiwa moto pamoja na mboga na matunda kama mabungo, topetope, machungwa au juisi.


