Chapati ya Malenge

Mapishi haya yanatumia mazao ya NUS ya jadi yanayochangia lishe bora kwa familia za Tanzania.

Mahitaji / Malighafi

Malenge (200g), unga wa ngano (800g), sukari (50g), chumvi (50g), mafuta (200ml)

Maandalizi

1. Chemsha malenge na yabarde.
2. Punja na changanya na unga, sukari na chumvi.
3. Ongeza maji ya malenge yaliyochemshwa, kanda unga laini, kisha kata mipira. Acha ipumzike, kisha tandaza umbo unalopenda (mstatili, mraba, mduara).
4. Kaanga kwenye kikaango pande zote mbili hadi yawe ya dhahabu.

← Mapishi yote